Watu 8 wafa katika ajali ya ndege Ujerumani

 
Watu wanane wamekufa baada ya ndege mbili ndogo kugongana angani kiasi kilometa 30 kaskazini mwa mji wa Frankfurt.

Polisi wa eneo hilo wamesema watoto wanne ni miongoni mwa waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea karibu na mji wa Wolfersheim.

Hata hivyo, chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahimika hadi sasa. Inaaminika kuwa hiyo ni ajali mbaya ya ndege kutokea nchini Ujerumani katika miaka ya hivi karibuni.
Previous
Next Post »