Tume ya uchaguzi yatangaza matokeo Misri


Rais wa Misri Mohammed Musri ametia saini kuwa sheria rasimu mpya ya katiba ambayo imeandikwa na makundi ya Kiislamu nchini humo na kusema itasaidia kumaliza mzozo wa kisiasa na kumruhusu kuelekeza mtazamo wake katika kuushughulikia uchumi ambao unalega lega.

Rais Mursi amefanya hivyo baada ya tume ya uchaguzi nchini Misri kutangaza matokeo rasmi ambapo theluthi mbili ya wapiga kura wameidhinisha katiba ya nchi hiyo. Kura ya ndio, ambayo imeidhinishwa na wapigakura wapatao asilimia 33 waliojitokeza kupiga kura , inasafisha njia kwa ajili ya uchaguzi wa bunge katika muda wa kiasi ya miezi miwili ijayo.
Viwango vya muda mrefu vya ukopaji nchini Misri vimepunguzwa na shirika linalopanga viwango la Standard and Poor's siku ya Jumatatu. Jana Jumanne , maafisa walitangaza hatua mpya za kuzuwia kuhamishwa kwa fedha kwenda nje ya nchi. Waziri mkuu Hisham Kandil amesema kuwa juhudi hivi sasa zitaelekezwa katika upunguzaji wa nakisi katika bajeti ya taifa na kuimarisha uchumi.
Previous
Next Post »