Sita wauawa nchini Misri

Watu sita ikiwa ni pamoja na mwandishi habari, wameuawa kwenye mapambano kati ya wapinzani na wafuasi wa rais wa Misri Momahed Mursi nje ya kasri lake. 

Duru za hospitali zinasema takribani watu 350 pia wamejeruhiwa, baadhi yao vibaya. Wakati huo huo jeshi la Misri leo limetuma vifaru nje ya kasri la rais baada ya usiku kucha wa mapambano makali. 

Takribani vifaru viwili na magari matatu ya kijeshi yamewekwa nje ya lango kuu la kasri kaskazini ya Cairo, wakati mamia ya wafuasi wa Mursi wakiimba nyimbo za kumuunga mkono rais. Wapinzani wamesema wataendelea na maandamano hadi pale rais Mursi atakapofutilia mbali   kura ya maoni kuhusu katiba mpya yenye utata inayopangwa Desemba 15. 

Hofu baina ya waislamu wenye itikadi kali na upinzani imekuwa ikiongezeka tangu Mursi alipoidhinisha amri inayomlimbikizia madaraka mnamo Novemba 22 na kuharakisha katiba mpya.
Previous
Next Post »