Aliyekuwa waziri wa kwanza mwanamke wa sheria nchini Ufaransa, Rachida Dati amedaiwa kuwa hajui nani ndiye baba wa mtoto wake kwakuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wanane kwa kipindi kimoja. | ||
Rashida Dati mwenye umri wa miaka 47 amedaiwa kuwa alikuwa bize kwenye kubadilisha mabwana kiasi cha kwamba hajui ni mwanaume gani ndiye aliyempa mimba. Dati amemfikisha mahakamani bilionea Dominique Desseigne, 68, akidai ndiye baba wa binti yake Zohra kufuatia uhusiano wao wa kimapenzi mnamo mwaka 2008. Desseigne amegoma kupima DNA akisema kuwa yeye alikuwa miongoni mwa wanaume wanane waliokuwa wakitembea na waziri huyo wa zamani wa sheria nchini Ufaransa. Katika ushahidi wa maandishi uliotolewa na wanasheria wa bilionea Desseigne umeweka wazi kuwa Dati alikuwa na mahusiano na wanaume wanane katika kipindi kimoja na imewataja wanaume hao kuwa miongoni mwao yumo aliyekuwa waziri mkuu wa Hispania, Jose Maria Anzar na aliyekuwa rais wa Ufaransa, Sarkozy. Pia katika listi hiyo yumo kaka wa rais huyo wa Ufaransa na pia yumo mwanasheria mkuu wa Qatari na matajiri wengine maarufu. Sheria za Ufaransa zinamruhusu mtu kugoma kupima DNA kwenye kesi kama hizi za madai ya watoto. Dati alichaguliwa kuwa waziri wa sheria mnamo mwaka 2007 lakini alifukuzwa kazi mwaka 2009 baada ya kuonekana utendaji wake wa kazi ni mbovu. | ||
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon