Mkuu wa majeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea kufuatia madai kuwa aliwauzia silaha makundi ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi hiyo.
Ripoti moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu, Generali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa wawindaji haramu na makundi ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia Mutomboki.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo amesema, maafisa kadhaa wa jeshi pia wanachunguzwa.
Serikali ya Rais Kabila imemfuta kazi mkuu huyo wa majeshi, siku chache baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi hao mpia wameutekja mji wa Sake, lakini msemaji wa serikali Lambert Mende, amesema wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuumboa tena mji huo mdogo.
Waasi hao ambao wanaaminika kuungwa mkono na serikali za Rwanda na Uganda, wametishia kuendeleza mapigano hayo hadi mji mkuu wa Kinshasa, ikiwa rais Joseph Kabila hatabuli kuanzisha mazungumzo ya amani.
Mazungumzo ya Amani
Uganda inaandaa mkutano wa marais wa Rwanda na Uganda hii leo na kuna ripoti kuwa baadhi ya viongozi wa kundi hilo la waasi wa M23 wamesafiri mjini Kampala kushiriki katika mazungumzo hayo.
Ripoti iliyoandikiwa Umoja wa Mataifa na kundi moja wa wataalamu huru, imesema kuwa Generali Amisi, anaendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa makundi ya kihalifu na waasi wanaohudumu Mashariki mwa Congo, eneo ambao bado kuna idadi kubwa ya wapiganaji wa waasi.
Hata hivyo kundi hilo la M23 halikuwa miongoni mwa makundi yaliyotajwa kwenye ripoti hiyo lakini kundi la Raia Mutomboki, moja ya makundi kadhaa yanayojumuisha wapiganaji wa Mai Mai, inaaminika kuwa na uhusiano wa karibu na kundi hilo la M23.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imenadi kuwa Generali Amisi aliagiza bundi 300, aina ya AK-47 kukabithiwa kundi moja linalohudumu katika eneo hilo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lijulikanalo kama Nyatura.
Ripoti hiyo imeongeza kusema kuwa waasi hao wananunua risasi kutoka kwa nchi jirani ya Congo na kusafirisha kupitia Kinshasa hado Mashariki mwa nchi hiyo na mtandao unaoendeshwa na washirika wa Generali Amisi, wakiwemo baadhi ya jamaa ya familia yake.
EmoticonEmoticon