KIPINDI KIPYA CHA LUNINGA CHA’DIARY YA LADY JAY DEE’ KUTOA SOMO KWA WASANII CHIPUKIZI NA CHANGAMOTO ZA KUWA MSANII BORA



Muimbaji mahiri wa kike hapa nchini Judith Wambura (kulia) almaarufu kwa jina la Lady Jay Dee akizungumza na waandishi wa habari leo katika mgahawa wake wa ‘Nyumbani Lounge’ uliopo jijini Dar es Salaam na kutambulisha rasmi kipindi chake kipya cha luninga kitakachoitwa‘Diary ya Lady Jay Dee’.
Amesema madhumuni ya kipindi hicho ni kuleta burudani tofauti kwa wapenzi wa muziki wake na muziki wa kizazi kipya kwa ujumla, vilevile kitatoa fundisho na changamoto kwa wasanii chipukizi kujua wasanii wakongwe wamepitia katika vikwazo gani.
Lady Jay Dee amesema kipindi hicho kitaonyeshwa ndani ya East Africa Television kuanzia tarehe 18 Novemba mwaka huu kila siku ya Jumapili.
Aidha ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kushiriki katika kudhamini vipindi vinavyobuniwa kama hivyo ili kuweza kutoa ajira kwa wasanii na wadau wengine wa sekta ya muziki na burudani.Kushoto ni Mkuu wa Vipindi wa East Africa TV Bi. Lydia Igarabuza
Mkuu wa Vipindi wa East Africa TV Bi. Lydia Igarabuza akizungumzia jinsi stesheni hiyo ilivyopokea kwa shangwe kipindi hicho na kuwa kitakuwa hewani Jumapili saa 3 usiku kuanzia Novemba 18 na kuwataka vijana wa Afrika Mashariki kukitazama ili kujifunza mengi kutoka kwa watu ambao tayari wanamafanikio kupitia tasnia ya muziki.
Previous
Next Post »