Jumla
ya Askari 10 wa jeshi la Wananchi wa
kambi ya 44KJ Mbalizi Wilaya ya Mbeya wanashikiliwa na jeshi lapolisi kwa tuhuma
za kuhusika na kifo cha Petro Sanga (25) mkazi wa chapakazi Mbalizi aliyeuwawa
kwa kuchomwa kisu shingoni na mdomoni.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman alisema kuwa tukio hilo lilitokea
Novemba 18,2012 majira saa 3:00 usiku katika grocery iitwayo Vanenemwe ambapo
marehemu alikuwa katika gocery hiyo alipochomwa kisu shingoni na mdomoni na
kufariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospiali teule ya Wilaya ya
Ifisi Mbalizi.
Alisema
kuwa marehemu alijaribu kuokoa uhai wake
kwa kukimbia toka eneo hilo hadi katika grocery hiyo lakini watu hao
walimkimbiza hadi eneo hilo na kumjeruhi vibaya kwa kumchoma kisu shingoni na
mdomoni.
Kamanda Athumani alisema kuwa chanzo cha tukio
hilo ni kulipiza kisasi kufuatia askari
jeshi mmoja aliyetambulika kwa jina la
Godfrey Matete wa kikosi cha 44KJ Mbalizi kupigwa na walinzi wa kilabu cha
pombe za kienyeji kiitwacho DDC kilichopo Mbalizi waliokuwa lindoni novemba
17,2012 majira ya saa 01:30 usiku.
Aidha alisema kuwa katika siku hiyo watu wengine sita walijeruhiwa kwa kupigwa sehemu mbali mbali za miili yao na wanaodaiwa kuwa ni askari wa JWTZ na kupatiwa hati ya matibabu na kati yao watatu walilazwa katika hospitali teule ya ifisi .
Alisema
kuwa katika vurugu hizo mali zawatu ziharibiwa ambazi ni pamoja na gari T.106
AWB iana ya Toyota Vista mali ya Paulo Maximililian iliyokuwa imevunjwa kioo
cha mbele,gari T884 auu Toyota Cresta mali ya Alile Godfrey lilivunjwa Side
Mirror upande wa kulia.
Kamanda
Athuman alisema kuwa Mwili wa marehemu
ulifanyiwa uchunguzi na daktari
wa serikali na kisha kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajiliya taratibu za mazishi na
kwamba uelelezi wa tukio hilo unaendelea
kufanyika.
Kamanda huyo ametoa wito kwa
jamii kuepuka tabia ya kujichukulia sheria mkononi na pindi wanapotendewa
isivyo halilali ni vizuri kutoa malalamiko yao katika mamlaka husika na ametoa
pole kwa ndugu jamaa na marafiki wa
marehemu Petro Sanga kwa msiba mzito
uliowakuta na kuwataka kuwa na moyo wa
subira katika kipindi hiki kigumu walichonacho.
EmoticonEmoticon