JESHI la polisi Mkoani Mbeya
limewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kuwafichua watu wanaojihusisha na
uuzaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake
kutokana na athari zinazojitokeza kwa vijana.
Akizungumza na wandishi wa habari
ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani mbeya Athuman diwani alisema kuwa
kumekuwa na tabia ya wananchi kujihusisha na kilimo cha bangi na uuzaji katika
wilaya ya chunya na hivyo kupelekea kushamili kwa biashara hiyo kwa kipindi cha
hivi karibuni.
Aidha alimtaja mkazi wa kijiji cha
makongorosi wilayani chunya mkoani mbeya Gineneka Charles(18) anashikiliwa na
polisi kwa tuhuma za kupatikana na gramu 500 za bangi.
Diwani alisema kuwa mtuhumiwa huyo
alipohojiwa alikiri kujihusisha na biashara na bangi na kwamba anatarajia
kufikishwa mahakani wakati wowote kujibu tuhuma zinazomkabili.
Awali katika tukio la pili watu
wanne wanashikiliwa na polisi wakazi wa kijiji cha madibila wilayani mbarali
mkoani mbeya kwa tuhuma za kupata na nyara za serikali
Diwani aliwataja wanaoshikiliwa na
kufikishwa mahamkamani kuwa ni
Kelius mhanga(40) msafiri njiwa (33) charles
kapemba(25) na martin Musinge (28 ) alisema watuhuumiwa wote kwa pamoja
walikamatwa na polisi waliokuwa doria wakiwa na nyama ta tembo kilo 10, nyati
kilo 15 na wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani.
EmoticonEmoticon