Hakuna feeling nzuri kwa mwanamke kama ile ajisikiapo wakati anapomwangalia mtoto wake mchanga aliye na siku ama wiki kadhaa baada ya kujifungua salama.
Ni hisia ambazo humpa furaha ya kutambua kuwa yeye ni mwanamke shujaa na asiye na mapungufu baada ya kujaaliwa kubeba ujauzito na kupata mtoto anayepumua.
Kwa Miss Tanzania wa zamani Jackline Ntuyabaliwe aka Klyinn ambaye ana wiki kadhaa tangu apate watoto mapacha ni hisia maradufu. Kwa mujibu wa tweet yake ya Jumatano hii, mrembo huyo amesema anafurahia kila dakika ya kuwa mama.
“Spending time with my sweet bundles of joy and loving every minute of motherhood.Im in love!”
EmoticonEmoticon