Kampuni kubwa ya mafuta ya Shell
inatarajiwa kufikishwa
mahakamani leo nchini Uholanzi, ikikabiliwa na mashtaka ya kuchafua
mazingira katika vijiji kadhaa nchini Nigeria.
Kesi hiyo imewasilishwa mahakamani na wakulima wanne wa Nigeria kwa ushirikiano na shirika moja la kutetea mazingira la nchini humo, Friends of the Earth.
Ni mara ya kwanza kwa kampuni kubwa ya Uholanzi inashtakiwa katika mahakama ya kiraia nchini humo kuhusiana na uharibifu uliotokea katika nchi ya kigeni.
Shell, inasisitiza kuwa haijaweza kusafisha eneo ambalo lilichafuka kutokana na shughuli zake nchini Nigeria.
Inasemekana kuwa nusu ya uvujaji wa mafuta katika eneo hilo imesababishwa na visa vya wizi.
Kesi hiyo inahusishwa na uvujaji wa mafuta uliotokea katika eneo la Ogoniland nchini Nigeria.
Wakulima wanasema kuwa mafuta yaliyovuja kutoka kwa mabomba ya mafuta ya kampuni hiyo, yameathiri mapato yao, kwa kuharibu mimea na mabwawa ya samaki.
EmoticonEmoticon