Uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini Mbeya
MENEJA
wa uwanja wa Sokoine uliopo jijini Mbeya Modestus Mwaluka amesema
maandalizi ya uwanja kwaajili ya ligi kuu ya Tanzania bara yamekamilika.
Amesema
yapo maboresho makubwa yaliyofanyika katika uwanja huo na sasa upo
katika kiwango cha ubora unaofaa kwa michuano mikubwa kama ligi kuu
inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi ujao.
Amesema
miongoni mwa maeneo yaliyofanyiwa ukarabati ni pamoja na eneo la
kuchezea(Pich) ambalo limejazwa udongo na kuoteshwa nyasi katika maeneo
yaliyokuwa na mabonde hali ambayo awali ilikuwa ikisababisha usumbufu
kwa wachezaji wakiwa katika mechi husika.
Meneja
huyo amesema kwa maboresho yaliyofanyika kwa sasa uwanja uko katika
hali nzuri na hata wachezaji wataona raha kuutumia tofauti na awali.
Kwa
upande wa masuala ya usalama,Mwaluka amesema kwa sasa usalama wa
wachezaji wawapo uwanjani,wale wa akiba pamoja na waamuzi na wahusika
wengine ni mkubwa kutokana na wigo uliopo ambao katika siku za mechi
ulinzi utaimarishwa zaidi ili mashabiki wasipate fursa ya kuingia eneo
lisilowahusu.
“Mpaka
sasa hatujapata ratiba lakini kwa taarifa tuilizonazo wakati wowote
kuanzia leo itatoka.Kwa upande wetu kama wamiliki na wasimamiaji wa
uwanja tumekamilisha mambo yote muhimu ikiwemo uboreshaji wa maeneo
korofi.Tunachosubiri ni kuanza tu kwa ligi” amesema Mwaluka.
Hata
hivyo baadhi ya wadau wa michezo jijini Mbeya wakiwemo wanahabari
wameshauri uongozi wa uwanja kwa kushirikiana na chama cha soka mkoani
Mbeya (MREFA) kuhakikisha unakuwepo utaratibu maalumu ambao hautaruhusu
mamluki kuvamia eneo la wanahabari.
Katika
ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu,mkoa wa Mbeya na mingine iliyopo
jirani itawakilishwa na timu ya Tanzania Prisons ya jijini hapa
iliyopata daraja baada ya kufanya vyema katika michuano ya ligi daraja
la kwanza iliyopita.
EmoticonEmoticon