Tamasha
la Tanzanite Sports Festival limeanza kutimua vumbi leo
Agosti 22
katika Uwanja wa Tandale Mji mdogo wa Tukuyu,Wilayani ya Rungwe Mkoani
Mbeya.
Mratibu wa tamasha
hilo Magige Flavian,amevitaja vituo mbalimbali ambavyo vitashiriki
tamasha hilo kuwa ni Morogoro Youth Academy kutoka Mkoa wa Morogo,
Zamaleki Sports Academy kutoka Mkoa wa Njombe na Mbeya Sports
Centre(MBASPO).
Vingine
ni Forest Youth Soccer Aspirants(Four ISSA),Majeshi Kids Soccer Academy
kutoka Mkoani Dar es salaam na Tukuyu Sports Centre ya Wilaya ya Rungwe
mkoani hapa.
Ameongeza
tamasha hilo litashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo riadha,mpira wa
pete,mpira wa miguu na michezo mingineyo mingi na vikundi mbali mbali
vya ngoma na wasanii mbalimbali watashiriki katika tamasha hilo.
Hata
hivyo Mratibu huyo Magige amesema lengo la tamasha hilo la Tanzanite
Sports Festival ni kukuza vipaji na kuchangia ujenzi wa Kituo cha
Rungwe.
EmoticonEmoticon