Dk. Kafumu aliibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga Tabora,uchaguzi uliofanyika Oktoba 2, mwaka jana.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, Mary Shangali, alisoma hukumu hiyo jana baada ya kuridhika hoja zilizowasilishwa na upande wa mlalamikaji kupitia aliyekuwa mgombea wa kupitia CHADEMA Joseph Kashindye
Jaji Shangali alisema kuwa Mahakama imeridhika na hoja saba za upande wa mlalamikaji, ambazo alisema zinathibitisha na kuonyesha kuwa uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Igunga haukuwa huru na haki.
Jaji shangali alizitaja baadhi ya kasoro zilizotengeliwa ushindi huo ni pamoja na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kutoa ahadi ya ujenzi wa daraja la Mbutu kwenye kampeni jambo ambalo ni kosa kisheria
Ikiwemo na Waziri huyo kuwatishia wapiga kura kwa kutumia nguvu kama wasipomchagua mgombea wa CCM basi daraja hilo halitajengwa
Ikiwemo na uzushi ulioenezwa na Mbunge wa Tabora Mjini, Bw. Ismail Aden Rage (CCM), kutangaza kuwa mgombea wa Chadema amejitoa katika uchaguzi huo jambo ambalo halikwua na kiungwana na kupotosha wapigakura.
Jaji Shangali aliongeza sababu nyingine kitendo kilichofanywa na Imamu wa Msikiti wa Ijumaa wa Igunga, Sheikh Swaleh Mohamed, kutangaza msikitini kuwataka waumini wa dini hiyo wasimchague mgombea kutoka Chadema
Hizo ni moja ya sababu zilizofanya Jaji Shangali kutengua matokeo hayo na kutangaza rasmi kutengua matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga na kuiagiza NEC kufuata taratibu za kufanya mchakato mwingine wa uchaguzi katika jimbo hilo.
Mara baada ya kutangazwa kwa hukumu hiyo wafuasi wa Chadema walijitokeza kuanza kushangilia kwa vifijo na nderemo

EmoticonEmoticon