Ripoti hiyo imesema kuwa wimbi la
joto lililokumba Marekani pamoja na ukame katika baadhi ya maeneo ya
Mashariki mwa Ulaya ndio chanzo kikubwa cha kupanda kwa bei hizo.
Bei ya nafaka kama vile mahindi ,ngano na maharagwe ndio ilipanda pakubwa kulingana na ripoti hiyo.
Benki hiyo sasa imeonya kuwa nchi ambazo hununua nafaka kutoka nje ndizo zitaathirika pakubwa.
Kuanzia mwezi Juni hadi Julai mwaka huu, bei ya
mahindi ilipanda kwa asilimia 25 wakati bei ya maharagwe aina ya soybean
ikipanda kwa asilimia 17. Ni bei ya mchele pekee ilishuka kwa asilimia
nne.
Nchini Marekani, ukame ulioripotiwa na kutajwa
kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya karibuni,
ulisababisha uharibifu wa mahindi na maharagwe wakati nchini Urusi,
Ukraine na Kazakhstan, ngano iliharibika sana.
Benki ya dunia pia imesema kuwa hatua ya kutumia
mahindi kuzalisha mafuta inawezekana ni mojawapo ya sababu ya kupanda
kwa bei ya mahindi nchini Marekani.
Nchi hiyo hutumia aslimia arobaini ya zao lake la mahindi kutengeza mafuta yanayotokana na mimea.
Kwa jumla, ripoti ya benki ya dunia kuhusu bei
ya vyakula ambayo hufanyia utafiti bei ya vyakula duniani, iligundua
kuwa bei ilipanda kwa asilimia sita zaidi mwaka huu ikilinganishwa na
mwaka jana.
EmoticonEmoticon