RAIS
John Magufuli leo anatarajiwa kupokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa
vyeti kwa watumishi wa umma katika Ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
Taarifa
iliyotolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais katika
Ikulu Ndogo ya Chamwino Dodoma, Jaffar Haniu ilisema taarifa hiyo
itawasilishwa kwa Rais Magufuli na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki.
Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma liliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba, 2016.
Hivi
karibuni wakati akifungua rasmi nyumba mpya za makazi ya wanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Rais Magufuli alisema anasubiri ripoti
kuhusu watumishi wa umma wenye vyeti feki wapatao 9000.
“…Kwa
hiyo mnaweza mkaona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi
hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa ni zaidi ya 56,000, kila mahali
unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima niyatatue matatizo kwa sababu
mlinichagua kwa ajili hiyo,” alisisitiza Rais katika hotuba yake hiyo.
EmoticonEmoticon