Vodacom
Tanzania Foundation yatoa msaada kufanikisha mchakato huo
Wahanga wa ugonjwa wa Satarani wanaotibiwa katika
taasisi ya Uchunguzi wa Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam
wataanza kunufaika na huduma bora kwa njia ya kisasa kwa kutumia Teknolojia ya
Mawasiliano kutokana na mchakato wa serikali kuimarisha huduma za taasisi hiyo.
Wakati jitihada hizo za serikali zinaendelea sekta
baadhi ya sekta binafsi zimeanza kuunga mkono jitihada hizo za serikali ambapo
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kupitia taasisi yake ya kuhudumia masuala ya
kijamii imetoa msaada wa kompyuta 10 za kisasa kwa taasisi hiyo.
Akiongea wakati wa kupokea msaada huo katika hafla
iliyofanyika hospitalini hapo leo,Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo,Dk.Julius
Mwaiselage,amesema kuwa msaada huu umepatikana katika kipindi mwafaka ambapo
hospitali hiyo iko katika mchakato wa kuendesha huduma zake kidigitali.
Dk.Mwaiselage alisema kuwa hivi sasa kumekuwepo na
ongezeko kubwa la wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa
uchunguzi na kutibiwa hivyo kuna umuhimu mkubwa kuhakikisha kuwa ili
kuwahudumia ni kuwa na huduma za kisasa katika kila idara kwa njia ya TEKNOHAMA
na tayari serikali na wadau mbalimbali wameanza kufanikisha mchakato huo.
Aliishikuru kampuni ya Vodacom kwa kuwa mstari wa mbele
kuunga mkono jitihada hizo “Tunawashukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa
kuunga mkono jitihada za kuboresha huduma zetu ili ziweze kuwa bora zaidi na
tunatoa wito kwa taasisi nyingine kuendelea kutuunga mkono katika mapambano
haya ya kutokomeza ugonjwa wa Saratani nchini na kuwapatia huduma bora wahanga
wa ugonjwa huu”.Alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa
Vodacom ,Jacquline Materu,alisema kuwa Vodacom kupitia taasisi yake ya
kuhudumia jamii ya Vodacom Tanzania Foundation imekuwa mstari wa mbele kuunga
mkono jitihada za serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye
jamii hususani katika kuboresha sekta ya elimu na afya.
“Leo tuko hapa kutoa msaada wa kompyuta 10 lakini
tumekuwa tukishiriki kufanikisha miradi mbalimbali ya afya ambayo imesaidia
kuokoa Maisha ya watanzania wenzetu hususani Wanawake na watoto wachanga na
tutaendelea kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha Maisha ya
watanzania “.Alisema.
Materu aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni mradi wa
ambulance wa kuwawahisha akina mama wajawazito katika vituo vya afya
wanapokaribia kujifungua,mradi wa kugharamia uchunguzi na matibabu wa
akina mama wahanga wa Fistula na Saratani,Mradi wa kusaidia vifaa kwa watoto
wanaozaliwa kabla ya umri na kufanikisha mafunzo mbalimbali ya watumishi wa
kada ya afya.
Mbali na kutoa msaada wafanyakazi wa Vodacom pia
wamekuwa wakijitolea muda wao kushiriki kusaidia miradi ya kijamii katika sekta
ya afya ikiwemo kutembelea mahospitalini na kutoa misaada kwa wagonjwa na
kuwapatia faraja.
Kwa upende wao baadhi ya wagonjwa waliolazwa
hospitalini hapo kupata matibabu wameshukuru wafanyakazi wa Vodacom kwa
msaada na kuwatembelea kwa ajili ya kuwapatia faraja.
EmoticonEmoticon