Serikali ya China imetoa ufadhili wa ujenzi wa uwanja wa Michezo kwa shule ya msingi Msoga iliyopo halmashauri ya wilaya ya Chalinze….
Akizungumza katika hafla ya kuoneshwa eneo patakapojengwa uwanja huo Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameishukuru serikali ya China kwa msaada huo kwakuwa Michezo ni Kitu muhimu kwa watoto huku akitoa rai kwa halmashauri ya chalinze kulinda eneo hilo …
Kwaupande wake mwakilishi wa balozi wa China amesema kuwa China inajivunia uhusiano mwema uliopo kati ya China na Tanzania,na watahakikisha wanajenga uwanja huo kwa wakati ili kuwapa fursa watoto kufurahia michezo.
Nae Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametoa rai kwa wananchi wake kuhakikisha eneo lililotengwa linalindwa ili dhamira ya china kujenga uwanja huo itimie
Ufadhili wa ujenzi wa uwanja huo wa michezo kwa watoto wa Msoga ni muendelezo wa ufadhili wa China katika kijiji cha Msoga baada ya kujenga shule ya msingi Msoga.
Rais
Mtsaafu wa awamu ya nne Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kulia)
akifafanua jambo kwa Mwambata wa Biashara kutoka Ubalozi wa China, Yang
Tong wakielekea kukagua eneo litakalojengwa viwanja vya michezo
Chalinze. Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani
Kikwete akiteta jambo na mpiga kura wake.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo ya eneo ambalo limepangwa
kujenga viwanja vya michezo kwa Rais Mtsaafu wa awamu ya nne Mh. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na Mwambata wa Biashara kutoka
Ubalozi wa China, Yang Tong (mwenye koti jeusi)
Mheshimiwa mbunge akiangalia moja ya jiwe la mpaka wa uwanja huo.
Ukaguzi wa eneo la viwanja ukiendelea. Wa kwanza kushoto kwa Mheshimiwa mbunge ni Diwani wa kata ya Msoga na Afisa Tarafa.
Mwambata wa Biashara kutoka Ubalozi wa China, Yang Tong akitoa salamu za ubalozi wa China kwenye mkutano huo.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akitoa neno la shukrani kwa serikali ya
China kwa misaada mbalimbali wanayoitoa kwa wanachalinze ikiwemo ujenzi
wa viwanja vya michezo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Sehemu ya wananchi wa Chalinze walioshiriki kwenye mkutano huo.
Raisi
mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi na viongozi
waliojitokeza kumpokea alipowasili kwenye viwanja vya Mwenge Msoga.
EmoticonEmoticon