Sheikh Nimr al-Nimr aliuawa baada ya kupatikana na makosa yanayohusiana na ugaidi
Somalia imetangaza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran ikiituhumu kwa kuingilia masuala ya ndani ya Somalia.
Serikali
ya Somalia imewapa maafisa wote wa ubalozi wa Iran mjini Mogadishu muda
wa saa 72 (siku tatu) wawe wameondoka nchini humo.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya mkutano wa baraza la mawaziri wa Somalia.
“Hatua
hii imechukuliwa baada ya kutathminiwa kwa kina na kutokana na hatua ya
Jamhuri ya Iran kuendelea kuingilia masuala ya ndani ya Somalia,”
taarifa kutoka wizara ya mashauri ya kigeni ya Somalia imesema.
"Jamhuri
ya Somalia inaitaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuheshimu uhuru wa
mataifa yote kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Mkataba wa Vienna kuhusu
Uhusiano wa Kidiplomasia wa mwaka 1961 na tamaduni za uhusiano wa
kidiplomasia.”
UN yashutumu kuvamiwa kwa ubalozi Iran
Ingawa
taarifa hiyo haijaeleza wazi, hatua hiyo inaonekana kuwa na uhusiano na
mvutano ambao umesababishwa na mauaji ya mhubiri wa Kishia nchini Saudi
Arabia.
Somalia
ni moja ya mataifa ambayo yalikuwa yameunga mkono hatua ya Saudi Arabia
kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran baada ya ubalozi wa Saudia
mjini Tehran kushambuliwa mjini Tehran.
Ubalozi huo ulichomwa moto na watu waliokuwa wakilalamikia kuuawa kwa mhubiri huyo Sheikh Nimr al-Nimr Jumamosi iliyopita.
Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran ulichomwa moto na waandamanaji
Mataifa
mengine washirika wa Saudi Arabia kama vile Bahrain, Sudan na Kuwait
yaliifuata Saudia katika kuvunja uhusiano wake na Iran.
Djibouti pia ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran ikionyesha kuunga mkono Saudi Arabia.
Alhamisi, Iran ilisema Saudi Arabia ilishambulia ubalozi wake mjini Sanaa, Yemen.
Iran na Saudi Arabia zimekuwa zikiunga mkono makundi pinzani katika mizozo inayoendelea nchini Syria na Yemen.BBC
EmoticonEmoticon