Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,
Jenista Mhagama, akizungumza na kamati ya maafa mkoa wa Singida na za
wilaya zake zote sita jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa
mkoa mjini hapa. Waziri Mhagama ameziagiza kamati zote za maafa kuanzia
ngazi ya kijiji kujenga utamaduni wa kufanya tafiti zitakazosaidia
kupambana na maafa katika maeneo yao.
Afisa
uchumi na uzalishaji sekretarieti ya mkoa wa Singida, Aziza Mumba,
akitoa taafita ya hali ya chakula mkoani hapa kwa Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista
Mhagama.Mumba alisema kwa msimu uliopita, mkoa ulikuwa na upungufu wa
chakula tani 104,672.
Mbunge
wa jimbo la Singida magharibi (CCM), Elibariki Kingu,akisisitiza jambo
kwenye mkutano ulioitishwa kwa ajili ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama,
kuzungumza na kamati za maafa ya mkoa na za wilaya zote sita.
Baadhi
ya wajumbe wa kamati ya mkoa na za wilaya sita za mkoa wa Singida,
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (hayupo kwenye picha).(Picha
zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu,
Jenista Mhagama, ameziagiza kamati za maafa kuanzia ngazi ya kijiji
kujenga utamaduni wa kufanya tafiti za kina juu ya matukio ya maafa
katika maeneo yao.
Mhagama
alisema tafiti hizo zitasaidia mno kamati za maafa za ngazi husika,
kufanya maandalizi ya kukabiliana au kuzuia maafa mapema, kabla ya
kuleta madhara.
Waziri
huyo ametoa changamoto hiyo wakati akizungumza na kamati ya maafa ya
mkoa na zile za wilaya sita, kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.
Akisisitiza,alisema
kamati za maafa zishirikishe wadau mbalimbali wakiwemo wazee katika
kufanya tafiti hizo,kwa madai kwamba ndio wanaofahamu vizuri mazingira
ya maeneo yao.
“Kwenye
vijiji au sehemu zingine zo zote,wakati na hasa wazee, wanajua mambo
mengi yakiwemo ya matukio ya maafa.Watu hawa wanajua baada ya miaka
mingapi,lazima njaa itokee au mvua kubwa zenye kuleta
maafa,zitanyesha”,alifafanua Mhagama.
Alisema
hayo ni baadhi tu ya maafa…lakini yapo maafa mengi zaidi ambayo
yanafahamika vizuri na wazee wa sehemu husika, na hayafahamiki kabisa na
kamati za maafa.
Waziri
huyo ambaye alikuwa akipita mkoani hapa akielekea Kahama,alisema kwa
hali hiyo upo umuhimu mkubwa kamati za maafa kushirikisha wadau/wazee
katika kufanya tafiti zinazohusu maafa.ili ziwe na tija zaidi.
Mhagama
amesisitioza zaidi,kwa kusema kuwa tafiti hizo ziainishe aina gani ya
maafa,yanatokea wakati upi.Pia tafiti hizo zisaidie kutoa tahadhari kwa
wananchi mapema ili wananchi waweze kujiandaa kukabiliana na maafa
husika.
Katika
hatua nyingine,waziri huyo alisema katika juhudi za serikali za
kuhakikisha hakuna Mtanzania atakaye kufa kwa njaa,imeongeza tani
zingine zaidi ya elfu tatu za nafaka kwa mkoa wa Singida,ili kupunguza
makali ya njaa.
“Huu
msada wa chakula kwa watu wenye upungufu wa chakula,utatumwa mkoani
kwenu wakati wo wote kuanzia sasa,Natoa onyo,chakula hiki kiwafikie
walengwa tu,ikibainika msimamizi amekwenda kinyume,huyo atakuwa
hajipendi”,alisema.
Awali
katibu tawala msaidizi,uchumi na uzalishaji sekretarieti ya mkoa wa
Singida,Aziza Mumba,alisema mkoa una upungufu wa chakula tani 104,672.
Alisema
kati ya tani hizo,tani 100,897 ni za kuuza kwa ajili ya kupunguza makali
ya bei,na tani 4,275 ni kwa ajili ya wananchi wasiojiweza.
Aidha,Mumba
alisema katika awamu ya mwezi huu,serikali kuu imetoa tani 328.7 za
chakula bure kwa watu wasiojiweza na tani zingine 2,958.3 kwa ajili ya
kupunguza makali ya bei ya chakula.
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo la Singida magharibi (CCM), Elibariki Kingu,
pamoja na kuipongeza serikali kuu kwa kuwajali wananchi wake ili wasife
njaa,ameiomba awamu hii ya tani zaidi ya elifu tatu,itumwe mapema
iwezekanavyo iweze kunusuru baadhi ya kaya ambazo hazina kabisa chakula.
EmoticonEmoticon