Wafanyakazi
wa Wizara ya Mambo ya Nchi wakiwa katika wamesimama nje ya jengo hilo
baada ya kutokea hitilafu ya cheche za umeme katika gholofa ya nne.
Wafanyakazi ambao walipata mshtuko wa ghafla wakiwa nje ya jengo hilo.
Baadhi ya
maofisa wa jeshi la polisi wanaofanya kazi zao katika jengo hilo la
wizara ya mambo ya ndani wakitoka nje baada ya hitilafu hiyo.
Msemaji
wa Jeshi la Polisi nchini, SSP, Advera Senzo Bulimba,akizungumza na
waandishi wa habari nje ya jengo la wizara ya mambo ya ndani ya nchi
baada ya kutokea cheche za moto katika jengo hilo katika gholofa ya nne
na kusema kuwa baada ya tukio hilo uongozi wa wizara hiyo waliwapigia
simu jeshi la zimamoto ambao walifika muda sahihi na kuangalia chanzo
cha moto huo na akaongeza kwa kusema kuwa hakuna mfanyakazi yoyote
katika jengo hilo aliyedhurika kutokana na cheche hizo za moto
zilizoonekana katika cyling board.
Gari la kikosi cha zimamoto likiwa katika eneo la tukio tayari kuzima moto endapo ungedhuru jengo hilo.
Wafanyakazi wa wizara hiyo wakiwa nje ya jengo, pembeni ni gari la zimamoto.
Mapema
leo asubuhi, jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam
lilinusurika kuwaka moto baada ya kutokea cheche za umeme ndani ya jengo
hilo na kuzua taharuki kwa watu waliokuwemo ndani ya jengo hilo kabla
ya Kikosi cha Zimamoto kufanikiwa kuudhiti moto huo.
EmoticonEmoticon