Waziri
Mkuu wa Côte d’Ivoire Daniel Kablan Duncan (hapa mwezi Novemba 2012)
ambaye Jumatano hii Januari 6 amejiuzulu na kuteuliwa kwa mara nyine
tena kuwa Waziri mkuu.
Na RFI
Rais wa
Côte d’Ivoire, Alassane Ouattara, Jumatano hii, amemteua kwa mara
nyingine tena Daniel Kablan Duncan kuwa Waziri mkuu wa nchi hiyo.
Bw. Duncan ameteuliwa baaada ya masaa machache ya kujiuzulu pamoja na serikali yake.
Mwishoni mwa mwaka 2015, Rais Alassane Ouattara alisema wazi kwamba serikali mpya imo mbioni kutangzwa.
Kabla ya
kujiuzulu Daniel Kablan Duncan, ambaye alimuandikia barua rais Alassane
Ouattara akimueleza kwamba heshima na sifa ya mawaziri mbalimbali
walioweza kuhudumu chini ya mamlaka yake: "Napenda kuwasilisha barua
yangu ya kujiuzulu kama Waziri Mkuu, na ile ya serikali", amesema Daniel
Kablan Duncan ambaye amehudumu kama Waziri mkuu tangu Novemba 2012.
Rais
Ouattara alipokea barua hiyo na kuishukuru timu nzima ya serikali yake,
akimsifu hasa Waziri wake mkuu anayemaliza muda wake kwa "umahiri wake
na uongozi wake"."Tunaanza muhula mpya ambao utaonyesha mwanzo mpya kwa
utekelezaji wa shughuli za serikali. Ni kazi yako ambayo ilipelekea raia
kuwa na imani na sisi", amesema rais Ouatttara, ambaye alichaguliwa
hivi karibuni kwa muhula wa pili.
Wadadisi
wanasema Daniel Kablan Duncan ameteuliwa kwa mara nyingine kwenye nafasi
ya Waziri mkuu kutokana na kazi nzuri alioifanya tangu Novemba mwaka
2012 alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kwenye nafasi hiyo.
Daniel
Kablan Duncan anatarajiwa kuunda serikali mpya, lakini haijafahamika
iwapo baadhi ya mawaziri waliohudumu katika serikali iliyopita
watateuliwa kwa mara nyingine kwenye nyadhifa walizokua wakishikilia.
EmoticonEmoticon