Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (kushoto) akimkabidhi mfano wa
hundi katibu mkuu wa Ambassador FC, Bakari Khalid kwa ajili ya
maandalizi ya ligi daraja la pili mkoa wa Shinyanga.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (kushoto) na Bakari Khalid Katibu
mkuu wa timu ya Ambassador wakati wa hafla ya kukabidhi msaada kwa timu
hiyo.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya kukabidhi hundi timu ya Ambassador FC.
Katibu wa timu ya Ambassador FC, Bakari Khalid akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi na Uongozi wa Mgodi wa Buzwagi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi katika hafla ya makabidhiano ya
hundi kwa timu ya Ambassador kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la
pili mkoa wa Shinyanga.
Vikosi vya timu za Buzwagi fc na Ambassador vikiwa katika maandalizi wakati wa ukaguzi kabla ya kuanza kwa mhezo.
Kikosi cha timu ya Ambassador fc
Kikosi cha timu ya Buzwagi fc.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (mwenye kofia) akisalimiana na
Nahodha wa timu ya Buzwagi, Saimon Sanga wakati wa mchezo wao wa
kirafiki na timu ya Ambassador FC.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (mwenye kofia) akisalimiana na wachezaji wa timu ya Ambassador FC.
Kikosi
cha timu ya soka ya mgodi wa Buzwagi kikiwa katika picha ya pamoja
wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa timu ya Ambassador FC. Katika
mchezo huo timu ya Ambassador FC iliibuka mshindi kwa kuwafunga wenyeji
wao Buzwagi FC, 2-1
Kikosi
cha wachezaji wa timu ya Ambassador FC ya mjini Kahama wakiwa katika
picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi na kampuni ya
uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi ulioko
wilayani Kahama.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mgodi
wa dhahabu wa Buzwagi umeikabidhi timu ya ambassador FC ya wilayani
Kahama kitita cha shilingi milioni kumi na laki tano kama sehemu ya
msaada kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki michuano ya ligi daraja la
pili ngazi ya mkoa - Shinyanga.
Msaada
huo ambao ulikabidhiwa na meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Mhandisi Asa
Mwaipopo umetolewa kwa timu hiyo ili kuiwezesha kufanya vizuri katika
michuano ya ligi daraja la pili inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi mfano wa hundi, meneja mkuu wa Buzwagi amesema
msaada huo kwa timu ya ambassador ni mwendelezo wa harakati zinazofanywa
na kampuni yake katika kuhakikisha makundi mbalimbali yanayozunguka
maeneo ya mgodi huo yananufaika na fursa mbalimbali zilizopo.
“Lengo
letu kubwa la kutoa msaada huu ni kutekeleza ahadi yetu ya kuisaidia
Jamii inayotuzunguka na tungependa kuona hata kupitia michezo vijana
wanajitengenezea ajira, kama mnakumbuka tumetoa udhamini kwa timu ya
Stand Utd inayoshiriki Ligi kuu ya Vodacom na sasa tumetoa msaada huu wa
fedha ili kuisaidia timu hii ili nayo iweze kufanya vizuri katika
mashindano yaliyo mbele yao”.alisema Mwaipopo.
Kwa
upande wake katibu wa timu ya Ambassador FC, Bakari Khalid ameushukuru
uongozi wa mgodi wa Buzwagi kwa msaada huo ambao amesema utasaidia
kuongeza hali ya mchezo kwa wachezaji wa timu yake.
“Natoa
shukrani kwa uongozi wa Buzwagi kwa msaada huu, niwaahidi kwamba sisi
kama Ambasador tutafanya vizuri nakuwa mabalozi wa kuitangaza Kahama
katika sekta ya michezo, kwani tunao vijana wazuri wenye uwezo wa
kucheza mpira na kwa kufanya hivi tunawahakikishia baadhi ya vijana
ajira kupitia michezo” Alisema Bakari.
Katika
hatua nyingine timu hiyo ya ambassador FC ambayo iko chini ya kocha
Karume Songoro ambaye amewahi kuzichezea timu za Yanga na timu ya taifa
ya Tanzania, ilimenyana na timu ya mpira ya Buzwagi mchezo ambao uliisha
kwa Ambassador iliibuka na ushindi wa goli 2-1.
EmoticonEmoticon