Madaktari kutoka taasisi ya Tiba ya kituo cha Catalan kilichopo Barcelona, wametangaza kugundua tiba ya Ugonjwa wa UKIMWI ambayo wamedai ni ya Uhakika.
Hatua hiyo inakuja baada ya takwimu kuonesha kuwa, kuna zaidi ya wagonjwa milioni 34 wanaougua ugonjwa huu hatari duniani.
Kwa mujibu wa daktari wa zamu aitwae Rafael Duartel, amesema walichukua damu ya vitovu ya mtu ambaye haina uwezo wa kupokea virusi vya VVU, kisha kumpandikiza mgonjwa wa UKIMWI na kumuacha kwa majaribio miezi 3 na kuthibitisha kuwa amepona kabisa ugonjwa huo.
Mkurugenzi wa tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania, amesema wapo tayari kushiriki kwenye majaribio hayo ila mpaka ithibitishwe na WHO.
EmoticonEmoticon