TRA yaamuru wafanyakazi wake kutoa taarifa za mali na madeni yao

atika hatua ya kurahisisha upelelezi unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi kufuatia ufisadi wa makontena 349, sasa jeshi hilo kupitia kwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA wameamuru wafanyakazi wote wa TRA kuwasilisha taarifa ya madeni na mali zao wanazo miliki ndani na nje ya nchi.
Amri hiyo imeelekeza kuwa, wafanyakazi wanapaswa kutoa taarifa kuanzia Disemba 2 hadi Disemba 15 na mfanyakazi yeyote atayekiuka amri hii atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
TRA
Aidha, amri hiyo imetoa angalizo kwa wafanyakazi wote wa TRA kuwa, taarifa zitakazo tolewa ziwe sahihi kabisa bila kupotosha chochote kuhusu mali na madeni ya mfanyakazi.
Katika kusisitiza hilo, taarifa imetoa onyo kali kuwa endapo mfanyakazi atapotosha kuhusu mali zake na madeni, basi hatua kali za kinidhamu zitafuata dhidi yake.
Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng