KISUKARI ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.
Njia zinazofuata ni za kujiepusha na ugonjwa huo:

1. Pimwa kiwango cha sukari kwenye damu ikiwa una uwezekano mkubwa wa kupata kisukari.
Kulingana na ripoti mbalimbali, karibu watu milioni 316 duniani pote wana kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu; ingawa wengi wao hawajui wana kiwango hicho. Kwa mfano, nchini Marekani pekee asilimia 90 ya watu wenye sukari nyingi kwenye damu hawatambui kama wana tatizo hilo.
2. Kula vyakula vyenye lishe.
Unaweza kufaidika ukifany amambo yafuatayo: Punguza kiasi cha chakula unachokula.
Badala ya kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi au vinywaji vyenye kaboni kama vile soda, kunywa maji, chai, au kahawa. Kula vyakula vya nafaka ambayo haijakobolewa badala ya vyakula vilivyochujwa sana viwandani.
Kula nyama isiyo na mafuta mengi, samaki, njugu, karanga, na maharagwe.
3.Fanya mazoezi.
Kufanya mazoezi kunaweza kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu na kukusaidia uwe na uzito unaofaa. Mtaalamu anapendekeza kupunguza muda unaotumia kutazama televisheni ili uwe na muda wa kufanya mazoezi. Huwezi kubadili chembe zako za urithi, lakini unaweza kubadili maisha yako. Utafaidika sana ikiwa utajitahidi kutunza afya yako.Chanzo CRI Swahili

EmoticonEmoticon