MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ameamuru kusitishwa mara moja malipo yanayofanywa kwa makandarasi waliojenga barabara tano za ndani ya wilaya hiyo.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ameamuru kusitishwa mara moja malipo yanayofanywa kwa makandarasi waliojenga barabara tano za ndani ya wilaya hiyo.
Amefanya hivyo kwa maelezo kuwa watendaji wa Manispaa hiyo, wameshirikiana na makandarasi hao kuiibia serikali Sh bilioni 5.7. Fedha hizo ni ongezeko ambalo makandarasi hao, wanatakiwa kulipwa baada ya kujenga barabara hizo, ambazo thamani halisi ya ujenzi huo ni Sh bilioni tano.Lakini, katika hali isiyo ya kawaida, makandarasi hao wanatakiwa kulipwa Sh bilioni 10, ongezeko ambalo ni zaidi ya asilimia 100. Akizungumza jana Dar es Salaam, Makonda alisema taratibu za Serikali zinataka kama barabara haikukamilika ndani ya muda uliowekwa kwa sababu mbalimbali, ikiwemo mvua na sababu zinginezo, mkandarasi anatakiwa kulipwa fedha zaidi ambazo ni asilimia 15 ya thamani ya fedha za mradi.“Lakini kinachostaajabisha katika miradi hii ya barabara, fedha ambazo zimeongezeka ni zaidi ya asilimia 15, kiasi hiki ni zaidi pia ya asilimia 100, wametumia utaratibu gani kulipa fedha hizi za ziada kwa makandarasi hawa?” Alihoji Makonda.

Previous
Next Post »