Kwa AY ni tofauti, na ndio maana bado ameendelea kuwa msanii anayeheshimiwa zaidi si tu na mashabiki, bali wasanii wenzake pia.
Rapper
huyo ambaye yupo nchini Afrika Kusini, alipost picha kwenye Instagram na
Facebook akiwa amezishika tuzo za MTV alizoshinda Diamond hivi karibuni
na kuandika:
Nilichokuwa
nakipigania tangu mwanzo nazidi kuona matunda yake na najisikia faraja
sana. Sasa kabla hazijatua Tanzania lazima tuzibariki kwanza,Congrats
once again Diamond Platnumz kwa awards hizi kubwa za #MTVEMA2015.
Mambo makubwa ya kushtukiza yatakujia soon
Mashabiki wamemsifu AY kwa moyo wake huo. Tazama baadhi ya comments:
Richard Claud
Napenda
sana ulivyo na roho isiyokuwa na wivu hata kidogo ndo maana unafanikiwa
kila siku siyo tu kimziki hata kibiashara na hustle zote unazozifanya.
Ulikuwa wa kwanza kushoot international video tukashangaa sana lakini
kumbe ndo ulikuwa unawaonyesha wasanii wenzako njia na nia ya kuthubutu.
Love u more our star..... #HolidaySeason hatari sana
Yussouf J. Magige
Wewe ndo
umeanzisha safari hii kubwa ya kujaribu kuutoa music wetu nje ya nchi na
kupitia wewe tumempata mwingine ambae ni diamond. Nawatakia kila la
heri wewe na wadogo zako ambao wana hamu ya mafanikio kama wewe.
Nawaombea sana
Juma Mkelemi Wasasa
A.Y! A.Y!
A.Y! A.Y! unique artist mwenye moyo wa upendo na ndomana pia kazi zako
2nazipenda hasa mm hapa nashangaa sana wasanii wengine kukicha wao ni
madongo2 kwa #Diamond why? kwan hzo 2zo amejipa? jaman fanz mm nampenda
xna A.Y namfatilia toka miaka ile ya #East_Coast nakumbuka 2005
nlipelekwa kwa mwenyekiti wa mtaa baada ya kumponda kipondo dogo
mwenzangu kwa kuiponda nyimbo ya #yule_by_A.Y mama alinilipia faini ya
Tsh.5000
EmoticonEmoticon