Zidane alipotezea ‘shavu’ la Madrid

Zidane anapigiwa chapua kuridhi mikoba ya Rafael Benitez ndani ya Real Madrid.
Zidane anapigiwa chapua kuridhi mikoba ya Rafael Benitez ndani ya Real Madrid.
Baada ya Los Blancos kufungwa kwenye mechi ya El Classico zimevuma tetesi kwamba Zinedine Zidane anatakiwa kuchukua nafasi ya Rafael Benitez kwenye klabu ya Real Madrid, jambo ambalo amelipinga mwenyewe.
Tetesi hizo zilipewa kasi baada ya mchezaji wa Brazil Rivaldo ku-post kwenye instagram yake kwamba ni wakati wa Real Madrid kumpa nafasi Zidane ajaribu ku-manage klabu hiyo kama Pep Gurdiola alivyopewa nafasi na Barcelona.
Kocha Rafael Benitez, anakabiliwa na shinikizo kubwa ndani ya kikosi cha Madrid baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo za La Liga.
Kocha Rafael Benitez, anakabiliwa na shinikizo kubwa ndani ya kikosi cha Madrid baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo za La Liga.
Waandishi wa habari wamemtafuta Zidane ambae ni kocha wa kikosi cha vijana cha Real Madrid ‘Castilla’ na yeye alijibu kama hivi, ‘Mimi ni kocha Castilla na Benitez ni kocha wa kikosi cha kwanza, mambo ni mazuri kwa sasa hapa Castilla.
Nitaendelea kuwa kocha wa Castilla kwa muda kwasababu nafanya vitu kidogo kidogo sina haraka. Kitu cha muhimu ni kuwa na furaha kwenye kazi unayoifanya na mimi nina furaha hapa ndani ya Castilla’.
Previous
Next Post »