Mshambuliaji Sergio Aguero alifunga goli katika kipigo cha 4-1 cha Manchester City kutoka kwa Liverpool.
Kwa sasa Kun Aguero anaongoza katika Ligi Kuu Uingereza kwa kuwa na magoli 85 kama mchezaji anayetoka Amerika Kusini.
Raia huyo wa Argentina, 27, amempiku mwenzake Carlos Tevez mwenye magoli 84.
Tevez aliwahi kuzichezea West Ham, Manchester United pamoja na Manchester City.
Wa tatu ni Luis Suarez mwenye magoli 69 aliyecheza misimu mitatu na nusu Liverpool kabla ya kutimkia Barcelona mwaka 2014.
Gus Poyet naye kutoka Uruguay anashika nafasi ya nne kwa kuwa na magoli 54.
WAFUNGAJI 10 WA AMERIKA KUSINI KUWAHI KUCHEZEA LIGI KUU UINGEREZA
Sergio Aguero Argentina-85
Carlos Tevez Argentina-84
Luis Suarez Uruguay-69
Gus Poyet Uruguay-54
Nolberto Solano Peru-49
Juan Pablo Angel Colombia-44
Hamilton Ricard Colombia-31
Juninho Brazil-29
Hugo Rodallega Colombia-29
Carl Cort Guyana-28
EmoticonEmoticon