TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 08.10.2015.
WATU
SABA WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA LORI KUFELI BREKI JIJINI
MBEYA.
WATU
SABA WAFARIKI DUNIA BAADA YA LORI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.617 AJP LENYE TELA T.656 BZQ AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKITOKEA
DAR ES SALAAM KUELEKEA NCHINI KONGO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE RAMADHAN HASSAN (31) MKAZI WA JIJINI
DAR ES SALAAM KUACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU.
WATU
WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO WAMETAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. RASHID MWAKIPOLOLO MIAKA KATI YA 17 – 22 2. MTOTO ROSE OSWARD (07) MKAZI WA SIMIKE 3. MARIAM MWAMEZE MIAKA KATI YA 23 – 25 4. GRACE MSIMBA (36) MKAZI WA ILEMI 5. FREDRICK MANYILA (17) MKAZI WA MBOZI NA WATOTO WAWILI, JINSI YA KIUME WENYE UMRI KATI YA MIAKA MITATU HADI
MITANO.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 07.10.2015
MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO ENEO
LA SIMIKE, KATA YA MABATINI, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO, WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. HAPPY WENER (31) MKAZI WA SIMIKE NA MTOTO SHADRACK JOSEPH (04) MKAZI WA
SIMIKE AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU.
CHANZO
CHA AJALI NI HITILAFU KATIKA MFUMO WA BREKI ZA GARI NA KUPELEKEA DEREVA
KUSHINDWA KULIMUDU KUTOKANA NA ENEO HILO KUWA NA MTEREMKO MKALI. DEREVA
AMEKAMATWA, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA
MADEREVA/WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI KUVIFANYIA SERVICE VYOMBO VYAO MARA KWA
MARA ILI KUWEZA KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA
WATEMBEA KWA MIGUU NA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUEPUKA KUKAA PEMBEZONI MWA
BARABARA KWANI NI HATARI KWA USALAMA WA MAISHA YAO.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R.
WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon