MZEE KINGUNGE NGOMBARE MWIRU AJITOA RASMI CCM


Mwanasisa Mkongwe wa Chama cha Mapinduzi na aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali za chama na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombare Mwiru ametangaza rasmi hivi punde kujiengua ndani ya chama hicho.

Ngingunge amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na kile alichoamini kuwa CCM haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa Misingi bora na waasisi wake. 

Aidha amesema hakusudii kujiunga na Chama Chochote cha Siasa nchini bali atakuwa mtanzania huru. 
Akizungumzia hali ya sasa kisiasa amesema kila kindi katika jamii hivi sasa linataka mabadiliko. 

Kingunge ametangaza uamuzi wake huo hivi pinde katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao unarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ITV. 
Previous
Next Post »