“PRESS RELEASE” TAREHE 16.10.2015.
·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA MTOTO
WAKE KUTOKANA NA MGOGORO WA KIFAMILIA.
·
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA JANGURUTU
AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBARALI.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DICKSON KAWAWA (50) ALIUAWA KWA KUPIGWA KWA VIPANDE VYA MATOFALI NA MTOTO WAKE
AITWAE SIKU DICKSON (20) MWENDESHA
PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA MWASHIWAWALA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.10.2015
MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA, KATA YA IWINDI, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
CHANZO
CHA KIFO HICHO NI KIPIGO NA KUTOKWA DAMU NYINGI BAADA YA MAREHEMU KUKATAZWA NA
MTOTO WAKE KUNYWA POMBE KWA MUDA MREFU NA KUKAIDI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA
UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MTU
MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA JANGURUTU WILAYA YA MBARALI AITWAYE JAILOS GOYAGE (56) AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA
ZA USAJILI T. 888 BRD AINA YA TOYOTA
LAND CRUISER IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE OMARY
NURU (36) MKAZI WA MPAKANI UBARUKU.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.10.2015
MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO
KIJIJI CHA JANGURUTU, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA
MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WANAFAMILIA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO. PIA ANATOA WITO
KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/MICHORO NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon