TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 18.09.2015.
·
WATU TISA WAFUASI WA CCM NA CHADEMA
WAJERUHIWA KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA MAENEO YA MBATA BUCHANI JIJINI MBEYA.
·
WATU WAWILI RAIA WA KIGENI WANASHIKILIWA
NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI KINYUME CHA
SHERIA.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MNAMO
TAREHE 17.09.2015 MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO ENEO LA MBATA –
BUCHANI, KATA YA GHANA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, MGOMBEA
UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CCM BW. SHAMBWE SHITAMBALA AKIWA NA WAFUASI WAKE, WAPENZI WA CHAMA
HICHO ALIKUWA AKIFANYA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA ENEO HILO KWA MUJIBU WA RATIBA
YAKE.
MGOMBEA
HUYO AKIWA KATIKA MKUTANO HUO, MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI
YA CHADEMA BW. JOSEPH MBILINYI
ALIKUWA AKIPITA ENEO HILO AKIWA NA MSAFARA WAKE KUELEKEA MAENEO YA NSOHO KWENYE
MKUTANO WA KAMPENI. KUTOKANA NA KITENDO HICHO WAFUASI WA CCM AMBAO WALIONEKANA
KUWA WENGI HADI ENEO LA BARABARA HIVYO KUPELEKEA MSAFARA WA BW. MBILINYI
KUTOWEZA KUPITA ENEO HILO HALI ILIYOPELEKEA KUZUKA KWA VURUGU ZILIZOPELEKEA
KUJERUHIWA KWA WATU NA UHARIBIFU WA MALI.
KUTOKANA
NA VURUGU HIZO, WAFUASI TISA WA VYAMA HIVYO VYA SIASA WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. ROBERT KERENGE (58) KATIBU WA CCM WILAYA YA MBEYA 2. SALUM MWANSASU (35) MKAZI WA MAJENGO
[CCM] 3. ATUPELE BROWN (39) MKAZI WA
GHANA [CCM] 4. ROSE NELSON (30)
MKAZI WA MAJENGO [CCM] 5. SAKINA SALUM
(25) MKAZI WA GHANA [CCM] 6. MALANYINGI
MATUKUTA (31) MKAZI WA FOREST [CCM] 7.
AGABO MWAKATOBE (44) MKAZI WA GHANA [CHADEMA] 8. JAILOS MWAIJANDE (23) MKAZI WA ITIJI [CHADEMA] NA 9. GABRIEL MWAIJANDE, DEREVA WA MGOMBEA
UBUNGE [CHADEMA].
AIDHA
KATIKA VURUGU HIZO GARI LA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA
CHADEMA BW.JODEPH MBILINYI AINA YA
TOYOTA LAND CRUISER YENYE NAMBA ZA USAJILI T.161
CPP LILIHARIBIWA KIOO CHA MBELE, TAA MOJA YA NYUMA UPANDE WA KUSHOTO NA
KIOO CHA UPANDE WA DEREVA KWA KUPIGWA MAWE. PIA PIKIPIKI ZENYE NAMBA ZA USAJILI
T.332 CHV AINA YA T-BETTER NA T.383
CSE AINA YA SKYMARK ZILIHARIBIWA KWA KUVUNJWA SIDE MIRROR ZA UPANDE WA KUSHOTO
NA ZIPO KITUO CHA POLISI KATI.
KWA
MUJIBU WA RATIBA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI ILIYOTOLEWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA
MBEYA KWA TAREHE 17.09.2015, ILIKUWA IKIONYESHA CHADEMA SAA 10:00 ASUBUHI HADI
SAA 15:00 ALASIRI WALITAKIWA KUFANYA MKUTANO KATA YA NSOHO NA SAA 15:00 ALASIRI
HADI 18:00 JIONI WALITAKIWA KUFANYA MKUTANO KATA YA MAENDELEO WAKATI CCM KWA
MUJIBU WA RATIBA WALITAKIWA KUFANYA KAMPENI KATA YA ITENDE SAA 08:00 ASUBUHI
HADI SAA 13:00 MCHANA NA SAA 13:00 MCHANA HADI SAA 18:00 JIONI MTAA WA MBATA,
KATA YA GHANA AMBAPO NIPO TUKIO HILI LILIPOTOKEA.
UPELELEZI
UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUPELEKA JALADA LA UCHUNGUZI KWA MWANASHERIA WA
SERIKALI ILI WALIOHUSIKA KATIKA VURUGU HIZO WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA IDARA NYINGINE,
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA WA NCHINI MSUMBIJI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ARQUEMIDES JOAO MAHANJANE (40) NA 2. HENRIQUES BENDITO ASSUBA (36)
WOTE WAKAZI WA MAPUTO WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI AMBAZO NI VIPANDE 2
VINAVYODHANIWA KUWA NI PEMBE ZA FARU ZENYE UZITO WA KILO 5 ½, VIPANDE 4 VYA MAWE
YADHANIWAYO KUWA NI MADINI YENYE UZITO WA KILO 1 ½ NA MZANI 01 [PORTABLE
ELECTRONIC SCALE].
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.09.2015
MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO
KASUMULU MPAKANI, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA
MBEYA WAKIWA KWENYE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI
ABL 860 MC AINA YA TOYOTA
HILLUX VIGO D/CABIN WAKITOKEA NCHINI MALAWI KUINGIA NCHINI. NYARA HIZO PAMOJA
NA VITU HIVYO VILIKUWA VIMEFICHA CHINI YA CHASES YA GARI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO
KWA WAKAZI WA MAENEO YA MIPAKANI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA
MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
Imesainiwa
na
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon