Manispaa
ya Ntwara Mikindani imewataadharisha wananchi wa wilaya hiyo na maeneo
mengine kuwa macho na matapeli walioibuka na kuwatapeli baadhi ya
wananchi fedha kwa madai ya kuwapatia kazi katika manispaa hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari kaimu mkurugenzi na afisa
utumishi wa manispaa hiyo Donald Nsoko amesema utapeli huo kwa sasa ni
mkubwa na watu zaidi ya watano wameripoti kuibiwa fedha na matapeli hao
hatua iliyowalazimu kufungua jalada polisi lenye namba MT, RB, 36/69
/2015 ili wakamatwe na kutiwa nguvuni.
Amesema matapeli hao wamekuwa wakibadilisha majina na
kujitambulisha ni afisa utumishi huku wakitumia lugha za kitapeli kuomba
fedha kwa minajili ya kuwapatia kazi.
Akizungumzia hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Henrry Mwaibambe
amekiri kupata malalamiko hayo huku akisisitiza utapeli huo pia
umekuwa ukifanyika katika kiwanda cha dangote kinachozalisha Cementi.
Hata hivyo kamanda mwaibambe amewaomba wananchi waliotapeliwa kutoa
ushirikiano kwa jeshi la polisi ili watu hao waweze kukamatwa na kutiwa
nguvuni.
EmoticonEmoticon