Kamati ya
masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti
mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza
nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira
wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni
mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia
mchezaji wa Azam FC John Bocco.
Nyoso
alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC
na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam,
kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu
mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Klabu ya
Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia
wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya
Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake
watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya
shilingi laki tano.
Wachezaji
waliopata kadi za njano wa Young Africans katika mchezo huo ni ni Salum
Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.
Aidha
klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000)
kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada
ya mchezo kumalizika.
Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.
Simba pia
inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia
waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo
nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
Mchezo
namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye
uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu
kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli
la upande wa kaskazini walitoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia
kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed
na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba
msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika
3.
Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
Mchezo
namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja
wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match
meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
Mchezo
namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye
uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na
Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote
zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
Mchezo
namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand
United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo
hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa
kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi
mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
Friends
Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume
27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza
wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya
mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni
i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said
Kwa
mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya
Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na
mwamuzi wa kati anapewa onyo.
EmoticonEmoticon