Siku chache zilizopita Rekodi ya mtu mfupi zaidi Duniani ilibaki wazi, aliyekuwa anashikilia Rekodi hiyo, Chandra Bahadur Dangi raia wa Nepal alifariki akiwa na umri wa miaka 75.. lakini Guinness World Records wameipata rekodi nyingine ya kuvutia.
Hawa ndio wapenzi warefu zaidi Duniani, majina yao ni Sun Mingming, mwanaume mwenye umri wa miaka 33 na mpenzi wake, Xu Yan
ambaye ana miaka 29 wote ni Raia wa China.. uhusiano wao ulianza
walipokutana kwenye Mashindano ya Michezo ya Kitaifa China mwaka 2009,
mwanaume ni mchezaji wa Basketball na mwanamke ni mchezaji wa handball.
Baada ya mambo kwenda sawa pande zote, walifunga ndoa mwaka 2013 na wako pamoja mpaka sasahivi, maisha yanaendelea poa japo moja ya changamoto kubwa wanayokutana nayo ni pale wanaposafiri kwenye basi, au ndege kupata siti za kuwatosha ni tatizo !!
Sun na mpenzi wake Xu wako Makao Makuu ya Guinness World Records ndani ya Uingereza ambapo rekodi yao itaingizwa pia kwenye Kitabu cha Rekodi za Guinness kitakachotoka mwaka 2016.
Sun Mingming
ana urefu wa futi 7.8 alafu mkewe ana urefu wa futi 6.1, kilichofanywa
ni kuujumlisha urefu wao kwa pamoja ambapo jumla yake inakuwa Futi 13.10
!!
Kipande cha video yao hii hapa
EmoticonEmoticon