Mkurugenzi Mtendaji wa Everjobs wa Ukanda wa Afrika Eric
Lauer, akiwaelezea waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa jinsi
mfumo wao wa tovuti ambao unaweza kuwaunganisha waajiri na waajiriwa kwa
urahisi kabisa huku waajiri wakipata nafasi ya kuweza kupata taarifa
zote muhimu kutoka kwa wanaoomba kazi kupitia tovuti hiyo pindi
wanapokuwa wamejiunga na Kampuni ya Everjobs Tanzania.Mkutano huo
ulifanyika jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar Es salaam.
Mkurugenzi wa Everjobs Tanzania, Florens
Roell akielezea namna ambavyo waajiri na waajiriwa wanaweza kunufaika
na Kampuni ya Everjobs Tanzania ambayo inatoa nafasi kwa waajiriwa
kuweza kuomba kazi kupitia tovuti yao ya www.everjobs.co.tz.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Everjobs Tanzania Lucas Masson (wa pili kutoka kulia) akielezea jinsi ya waajiliwa ambavyo wanaweza kujiunga katika tovuti yao ya www.everjobs.co.tz na kuweza kuona nafasi za kazi mbalimbali zinazotangazwa kupitia tovuti hiyo na kuweza kuomba kazi hapo hapo kupitia tovuti.
Mmoja wa wageni waalikwa akiuliza swali kwa Wakurugenzi na maafisa wa Everjobs wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa uliofanyika jana
Mkurugenzi Mtendaji wa Everjobs Katika Ukanda wa Afrika Eric
Lauer (wa kwanza kushoto) akijibu baadhi ya maswali yaliyokuwa
yakiulizwa na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa
waliohudhuria mkutano uliofanyika jana katika hoteli ya Serena Jijini
Dar
Mmoja wa wageni akitoa shukrani kwa wamuluki wa kampuni ya Everjobs Tanzania kwa kuona changamoto na kuifanya kuwa fursa.
Baadhi ya Wageni waalikwa na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo
EmoticonEmoticon