BEKI MANCHESTER UNITED AVUNJIKA MGUU AKIPAMBANA UHOLANZI

KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kwamba beki wake Luke Shaw atakuwa nje mwa muda usiopungua miezi sita baada ya kuumia jana katiia mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wenyeji PSV nchini Uholanzi.
Katika mchezo huo ambao United ililala 2-1, Shaw alimwaga machozi wakati wanatolewa nje kutokana na uchungu wa maumivu makali kutokana na kuvunjika mguu wake wa kulia.
Dunia ya soka iliungana usiku wa jana baada ya beki wa PSV Eindhoven, Hector Moreno kumvunja mara mbili mchezaji wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 20 mguu wa kulia.
Shaw aliwekewa hewa ya ziada na kupatiwa huduma ya kwanza uwanjani mjini Eindhoven kabla ya kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi. Atarejeshwa Manchester leo na Alhamisi anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.
Previous
Next Post »