Maria Mwandaaji
wa mashindano ya Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai alizungumza katika
mashindano yaliyopita.
Miss Universe Tanzania 2014 Caroline Bernard
akitoa elimu ya afya kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Msimbazi
Mseto.
********
Na Mwandishi
wetu
Mashindano
ya maarufu ya urembo duniani, Miss Universe, sasa yatakuwa chini ya kampuni ya
kusaka, kuendeleza vipaji na masoko
ijulikanayo kwa jina la WME/IMG.
Awali mashindano
hayo yalikuwa yakiendeshwa kwa ushirika baina ya kampuni hiyo na kampuni
inayojishughulisha na masuala ya habari na burudani ya NBCUniversal na
mtangazaji maarufu wa vipindi vya televisheni, mwanasiasa na mfanyabiashara,
Donald J Trump.
Akizungumza
jijini jana, Mwandaaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi
Tsehai alisema kuwa wamepokea taarifa kuhusiana na kampuni mpya hiyo ambayo pia
inaandaa mashindano ya Miss USA na Miss Teen Usa.
Maria ambaye
pia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Compass Communications alisema kuwa
wamepokea mabadiliko hayo na wataendelea kufanykazi na mmiliki huyo mpya ili
kuendeleza vipaji vya wasichana nchini.
Alisema kuwa
mashindano ya Miss Universe ni moja kati ya matukio makubwa ya burudani duniani
ambayo usaidia wasichana kutoka nchi zaidi ya 190 zinazoshiriki kila mwaka na
watu zaidi ya nusu bilioni kufuatilia mashindano hayo kwa njia mbalimbali
ikiwemo mitandao na televisheni.
“Kwa sasa
tupo katika maandalizi ya kufanya mashindano ya Miss Universe Tanzania,
tunaamini kuwa mabadiliko haya yatatupa changamoto zaidi kwa lengo la kufika
mbali na zaidi kuhakikisha tunatwaa taji baada ya matokeo mazuri ya Flaviana
Matata ya mwaka 2007 ambapo aliingia hatua ya 10 bora,” alisema Maria.
Afisa Mkuu
wa kampuni ya WME/IMG, Mark Shapiro ameahidi kuyaendeleza mashindano hayo
kufika ngazi ya juu kabisa ikiwa pamija
na washindano bora.
"Najisikia
faraja kuendshs mashindano haya, tutayaendeleza kwa kiwango kikubwa na
kuhakikisha umaarufu wake unaongezeka, naamini mashabiki wengi zaidi kwa sasa
watafuatilia mashindano yetu kwa njia ya mbalimbali,” alisema Shapiro.
EmoticonEmoticon