
Balozi
wa Luv touch Manjano Irene Pul Katika Picha ya Pamoja na washiriki wa
Semina ya ujasiriamlai ya wanawake kwa kupitia Vipodozi vya Luv Touch
manjano iliyochini ya Manjano foundation.Lengo la Mradi huo ni kuona
kwamba wanawake hawa wanajisimamia na kujikita vizuri kwenye Biashara ya
Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara zao kwa lengo la
kumuongezea ajira mwanamama na kuondoa dhana za ukosefu wa ajira kuwa
chungu ya yeye kujiwezesha katika kujikimu mahitaji yake ya msingi,
yaani aweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa kupitia
ujasiriamali.Balozi huyo amewashauri Washiri hao kwanza kupenda
ujasiriamali na kufanya kazi kwa bidii lazima watafanikiwa.Pili kila
mshiriki kuwa mbunifu kwenye biashara na kuja na kitu cha kipekee
ambacho kitawafanya watumiaji wa luv Toch manjano pamoja na wateja
wengine kushawishika kuwaunga mKono washiriki hao katika biashara yao
pamoja na kuwatangaza kwa watu wengine wengi zaidi.


EmoticonEmoticon