Mgombea
Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia
umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana,
Septemba17, 2015, katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama
Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni kwa ajili ya Jimbo
la Mtwara mjini, uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
jana, Septemba 17, 2015.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan
akipokea Wanachama waliohamia CCM, kutoka vyama vya CUF na Chadema,
wakati wa mkutano wa kapnei uliofanyika jana, Septemba 17, 2015 katika
mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
Kada
wa CCM, Mtela Mwampamba akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jana,
Septamba 17, 2015 katika mji mdogo wa Mikindani, Jimbo la Mtwara Mjini.
Msanii
wa Bongo Movie, Snura akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika
Septemba 17, 2015 katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
Vijana
wakiungana na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia
Suluhu Hassan kuishangilia CCM, baada ya kuwapokea kutoka vyama vya CUF
na Chadema katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana, Septemba 17,
2015.
Mgombea
Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia
mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Mafia mkoani Pwani, jana,
Septemba 17, 2015.
Aliyekuwa
Mbunge wa Mafia ambaye pia aliingia katika kinyan'ganyiro cha kuomba
ridhaa ya CCM kuwania tena ubunge wa jimbo hilo, Abdulkarim Shah,
akimnadi Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo, Mbarak Dau, katika mkutano wa
kampeni uliofanyika leo katika katika Kisiwa hicho cha Mafia.
Mgombea
Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza
Kada wa CUF, Mohamed Albadawi, baada ya kutangaza kuhamia CCM katika
mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani.
Albadawi awali alikuwa Mgombea Ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya
CUF baada ya kuongoza katika kura za maoni, lakini baadaye akaenguliwa
na chama hicho na kupachikwa, Shomari Kimbau ambaye alihamia CUF baada
ya kushindwa katika kura za maoni za CCM.
Mgombea
Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia suluhu (Kushoto),
akishiriki kucheza muziki wa taarab uliokuwa ukitumbuizwa na nguli wa
muziki huo, Mzee mwishoni mwa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika
jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
EmoticonEmoticon