Dunia ina mambo, wapo wanaokubaliana na
msemo kwamba umri ni namba tu na sio kitu cha kujali sana unapokuwa
kwenye suala la mapenzi.
Stori kwenye kurasa za Magazeti Uganda, kichwa cha Habari ni Ndoa ya Bibi wa miaka 70, Zaituni Nakanda na kijana wa miaka 27, Steven Tikubuwana…
wawili hao wana mipango ya kuwa na Ndoa halali kabisa mapema
iwezekanavyo mwaka 2016 na kwa sasa wanaishi pamoja tena kwenye nyumba
ya Chumba kimoja tu ambayo inamilikiwa na Zaituni !!
Steven anasema wazazi wake hawajui lakini iko mipango ya kuwakaribisha nyumbani kwao ambako wanaishi yeye na Zaituni, baadae wataendelea na mambo mengine ikiwemo mipango yao ya Ndoa.
Unajua love yao ilianzaje? >>> ‘Sikuwa na kazi na sikuwa hata na mahali pa kuishi kwa karibu miezi miwili. Alinikaribisha nyumbani kwake na tukaanza maisha’ >>> Hayo ndio majibu ya Steven Tikubuwana.
Baadhi ya ndugu na watu wa karibu hawakubaliani na uamuzi wa Steven kuwa na uhusiano na Bibi huyo lakini mwenyewe anasema hata haimuumizi kichwa !!
EmoticonEmoticon