Magufuli alivyopokelewa kwa kishindo Tabora



Magufuli alivyopokelewa kwa kishindo Tabora

2[1]
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitoa Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
3[1]
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa mji wa Tabora kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
4[1]
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo.
8[1]
Mgombea Ubunge wa jimbo la Nzega Vijijini Dk. Khamis Kigwangala akiwahutubia wananchi wa Nzega kwenye mkutano ulioongozwa na Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
10[1]
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega mjini akihutubia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ambapo mgombea wa Urais kupitia CCM alihutubia.
12[1]
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
26[1]
Wakazi wa Bukene wakimsikiliza mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Previous
Next Post »