Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa
Bariadi (hawapo pichani) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa
Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa
Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya
Uchaguzi hapa nchini. Katika ziara hiyo, Mh. Lowassa aliambatana na
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye pamoja na Mwanasheria wa
CHADEMA, Mh. Tundu Lissu.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa
Vyama vinavyounda UKAWA wa Mkoa wa Simiyu, wakati alipowasili kwenye
Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu,
kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika
Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini.
Waziri
Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akihutubia katika Mkutano wa
hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika
kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo,
leo Septemba 17, 2015.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bariadi,
Mkoani Simiyu, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara
wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya
Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Badiadi kupitia CHADEMA, Godwin Simba, katika Mkutano wa hadhara wa
Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi,
Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiagana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Badiadi kupitia CHADEMA, Godwin Simba, mara baada ya Mkutano wa Kampeni,
uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani
Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015. Katikati yao ni Waziri Mkuu wa
Zamani, Mh. Fredrick Sumaye na Kulia ni Mwanasheria wa CHADEMA, Mh.
Tundu Lissu.
EmoticonEmoticon