KATIBU
mkuu wa CHADEMA Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema aliamua kuachana
na CHADEMA na siasa kwa ujumla tangu tarehe 28/08/2015 baada ya Mbunge
wa Monduli Edward Lowasa kujiunga na CHADEMA, kwa kile alicho dai kuwa
asingeweza kushiriki kumsafisha mtu mwenye madhambi na badala yake
aliona ni vyema ajiengue kwakuwa yeye sio muumini wa siasa za ulaghai.
Kauli
hiyo ameitoa katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es
Salaam, amabapo amesema ameamua kayasema hadharani kwa kile alicho dai
kuna upotoshwaji unao endelea kuwa yuko likizo na kwamba atajiunga na
shughuli za chama hicho mbele ya safari, huku akidai kuwa hakuwa likizo
na wala hakupewa barua yoyote ya likizo
Hata
hivyo amesema alijaribu mara kadhaa kuandika baraua za kujiuzuru lakini
hakuweza kusikilizwa na mtu yoyote, na baadae aliamua kuchukua uamuzi
wa kuchana shughuli za chama hicho, na kwamba uvumi uliokuwa ukiendelea
kuwa Slaa amezuiwa na mke wake Josephine
ameongeza
kuwa kitendo cha kuwaruhusu baadhi ya wabunge waliotemwa na CCM baada
ya kura ya maoni nacho kimechangia kumuondoa katika chama hicho, huku
akimtolea mfano Waziri mkuu wa wazamani Fredrick Sumaye kuwa ndiye mtu
ambaye alikuwa na mgogoro nae baada ya kumuita fisadi katika bunge la
jamuhuri ya muungano wa Tanzania, amabapo na yeye leo hii ameendelea
kuwaita ni “MAKAPI” .
Naondoka
leo huku nikisikitika kuwa sura ya CHADEMA imebadilika nakuwa kama CCM,
sasa utawezaje kuleta mabadiliko nawatu wale wale wanaotuhumiwa na
kashfa zinao umiza taifa hili? Alisema Dkt Slaa.
Aidha
alimaliza kwa kusema amestaafu siasa ila hana chama chochote ila bado
ataendelea kuwatumikia watanzania kwa njia nyingine kwakuwa ana vipawa
alivyo barikiwa na mungu lakini amewataka wananchi kuto pumbazwa na
shamra shamra zinazo endelea badala yake wananchi wanatakiwa kutambua
kazi waliyo nayo kwa sasa.
KUHUSU LOWASA KUHUSIKA NA RICHMOND DKT SLAA AME ANIKA HAYA.
kifungu
cha 152 cha katiba ya nchi hii kina sema jukumu kubwa la waziri ndio
msimamizi wa shughuri za serikali sasa anawezaje kukataa kuwa yeye
hakuhusika?
Na
katika makampuni yaliyo omba zabuni ya Umeme mwaka 2006, kampuni ya
Ricmhond ndiyo kampuni pekee iliyokuwa na sifa “sifuri” haya yoote
anayajua na kama hajui basi alikuwa ni mzembe! na kama alikuwa mzembe
basi hafai kuwa Rais. alisema Dkt Slaa.
Na
aliagiza tenda ifanyike ndani ya siku 10, wakati sheria ya PPRA ina
tamka tenda yoyote inatakiwa ifanyike ndani ya siku 45, ni kinyume na
sheria.
Sasa hao wanao mtetea watoke hadharani kama mnaona sisi hatujui chochote, mbona mnata kutu pumbaza!?
-Asema sina tabia ya kuchengachenga nasimamia ninachokiamini
-Mengi yamesemwa na kuandikwa magazetini
-Sina ugomvi na kiongozi yoyote, maana siasa si ugomvi, sina chuki, sina hasira na mtu yeyote
-Siasa inayoongozwa na propaganda, ulaghai ni kuleta vurugu katika taifa na nimekataa hayo
yote.
-Ni kweli nilishiriki katika majadiliano tangu mwanzo
-Misingi niliyoweka ni kwamba Lowassa atangaze kuwa ameachana na chama chake na aeleze anakwenda chama gani kwanza na ajisafishe na tuhuma zake
-Asema hawezi kumsafisha mtu bila yeye kufanya hivyo
-Asema alihoji kama Lowassa anakuja Chadema kama faida au mzigo (assets au liability)
-Asema anataka mgombea mwenye uwezo, sifa na kuiongoza Chadema kuiondoa CCM.
-Kama ni assets anakuja na akina nani? vijana wa mitaani, bodaboda au watu wa aina gani? ni viongozi makini?
-Asema aliambiwa kuwa anahama na wabunge 50, wenyeviti wa mikoa 22, wenyeviti wa CCM wilaya 82.
-Sikupewa majina ya wabunge wala wenyeviti.
-Nikatakiwa kuitisha kikao nikaitisha lakini sikuwa na majibu kama Lowassa ni
Assets au Liability.
-Tangu 2004 sikuwahi kutofautina na mwenyekiti wangu bali tulitofautia kwa hilo.
– Asema aliandika barua ya kujiuzulu kwa M/kiti Prof. Safari barua ikachanwa.
-Siasa ni sayansi haitaki uongo wala ulaghai au propaganda
-Asema mke wake halipwi chochote kutoka Chadema na amekuwa akizunguka nchini kwa mshahara wa Dk. Slaa.
EmoticonEmoticon