Mratibu
wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga akizungumza
wakati akifungua kongamano hilo lililo washirikisha wadau mbalimbali
kwa kutoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku. (Picha na Geofrey Adroph).
Na Andrew Chale, modewjiblog
[Dar es Salaam] Chama cha Afya ya Jamii nchini (TPHA), kimeendesha
kongamano maalum kwa wanafunzi wa shule msingi zaidi ya Saba ndani ya
Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kutoa elimu ya madhara yatokanayo na
utumiaji wa bidhaa za Tumbaku pamoja na kujikinga na athari zake mbaya
baadae.
Akielezea katika kongamano hilo, Afisa wa TPHA ambaye pia ni msimamizi
na mtaafiti wa masuala ya kupambana na madhara ya Tumbaku, Dk. Bertha
Maegga amebainisha kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaendesha mradi
uliopewa jina la “80 CHILDREN STRONG” ukitoa elimu kwa vijana wadogo
wenye umri wa miaka 10-14, hasa wa shule za msingi.
Dk. Maegga akihutubia umati wa wanafunzi wa shule hizo saba katika
kongamano hilo lililofanyika shule ya Msingi Kijitonyama Visiwani,
aliwataka wazazi, walimu, walezi na jamii kuwalinda na kukemea watoto
wao kuachana na vitendo vya matumizi ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo
sigara, ugoro, shisha na Tumbaku yenyewe.
Aidha, amebainisha kuwa, wameweza kulenga kundi hilo kutokana na kuwa
na changamoto za kiukuaji wa kiakili na kisaikolojia.
“Umri huu kuna utundu na utukutu mwingi na akili nazo bado hazijakomaa
kuepuka ushawishi wa namna mbalimbali ukiwemo na wa matendo yasiyofaa
katika maisha yao ya baadaye.
Tukiweza kuwalinda katika umri huo. watabaki salama hadi
watakapojitambjua nafsi zao na kuamua mambo ya busara na salama katika
maisha yao ya baadae” alibainisha Dk. Maegga.
Mshauri wa masuala ya Afya na Familia, mgeni rasmi Dk. Ali Mzige
akizungumza kwa kutoa elimu kwa miongoni mwa watu walio weza kuhudhuria
kongamano hilo la uelimishaji kuhusu Tumbaku na matumizi ya yanayotokana
na bidhaa za Tumbaku.Kwa upande wake, Dk.
Ali Mzige mganga wa hospitali ya kimataifa ya Afya ya uzazi
ametoa elimu kwa vijana hao na kubainisha kuwa sigara, tumbaku, shisha,
ugoro na kuberi ni hatari kwa afya za mwili huku ikisababisha magonjwa
mbalimbali.Miongoni mwa magonjwa hayo
yatokanayo na matumizi ya sigara ambapo wanaoathirika zaidi ni vijana
kwa sababu ya kufuata mkumbo pamoja na kuhisi kwamba uvutaji wa sigara
unaongeza sifa ya kuwa mwanaume kamili kitu ambacho si kweli.Changamoto
kubwa ni kwamba serikali imeshindwa kudhibiti watengenezaji wa Sigara
kwa sababu wanapata kodi kutoka katika viwanda vya sigara japokuwa
mapato ni madogo kuliko madhara.
“Sigara ina kemikali 4000 ambazo zina
uwezo wa kusababisha magonjwa zaidi ya 40, ambayo ni pamoja na ugonjwa
wa moyo, kisukari, na saratani ya mapafu, saratani ya kinywa na
mengine mengi.
Tumbaku na Sigara zote zimekuwa na
madhara yanayofanana. Tumbaku imekuwa ikitumika hasa maeneo ya
vijijini na sigara watumiaji wengi wanatoka mjini” alieleza Dk.
Ali Mzige.
Kwa upande wao wanaharakati wa kupambana na
matumizi ya sigara kutoka chuo cha Tiba Muhimbili, kupitia taasisi yao
ya African Fight Cancer, Bernard Temba amewaelezea wannafunzi hao kuwa,
ni wakati wa kuepuka vishawishi dhidi ya watu wanaotumia sigara kwani
wasipofanya hivyo wataweza kupata madhara makubwa ya kiafya.
Mwalimu
Margareth William mshereheshaji katika siku hiyo ya kongamano la
uelimishaji vijana kuhusu Tumbaku na madhara yatokanayo na bidhaa zake.
Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Makumbusho
ambaye pia alikuwa mgeni katika kongamano hilo, alitoa wito kwa walimu
na wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao ikiwemo kufuatilia nyendo zao
mara kwa mara ili kuwakinga na vishawishi hivyo vya matumizi ya bidhaa
zitokanazo na tumbaku kwani zina madhara makubwa hasa kwa afya za watoto
wadogo.
Mradi huo wa ’80 Children Strong’,
unaosimamiwa na Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) unafadhiliwa na
Shirika dogo la Conquer Cancer Foundation ambalo linahusiana na
American Society for Clinical Oncology (ASCO) ya nchini Marekani
(Chama cha kitabibu cha masuala ya uchunguzi wa tiba ya saratani.
Hata hivyo, TPHA imedhamiria kuwa kila
mtoto anapata haki ya kuelimishwa kujikinga na matumizi hayo mabaya ya
tumbaku, ambapo kwa darasa la watoto 80, asiwepo hata mmoja
atakayeingia kwenye viashiria vibaya vya matumizi ya tumbaku hivyo
wataendelea kutoa elimu hiyo sehemu mbalimbali nchini.
Kwa upande wa shule hizo zilizohudhuria
kongamano hilo ni pamoja Shule ya Msingi Mapambano, Kijitonyama
Visiwani, Victoria, Mwananyamala B, Mwananyamala Kisiwani, Mashujaa,
Shekilango na Mapambano.
Kwa upande wa watoto hao walipata pia
wasaha wa kuuliza maswali na kupatiwa majibu huku pia kukifanyika na
masuala ya maigizo, ngoma, shahiri na ngonjera zilizokuwa na jumbe
mbalimbali za kupambana na matumizi ya tumbaku.
Wanafunzi wakisoma na kuelekezana jarida lililochapishwa mahususi kwa ajili ya kuelimisha matumizi mabaya ya Tumbaku.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mashirika na vyuo mbalimbali.
Kikundi
cha majigambo ya jukwaani (ngonjera) kikitoa ujumbe kwa wageni waalikwa
pamoja na wanafunzi wenzao kuhusiana na kupambana na kudhibiti matumizi
hatari ya Tumbaku.
Wanafunzi
wakionesha vipaji vyao vya kuigiza kwa kuelimisha kuhusiana na na
madhara ya Tumbaku na ni namna gani ya kuweza kujikinga.
Bernard
Temba kutoka Chuo cha Afya cha Muhimbili akitoa somo kwa wanafunzi wa
shule za msingi zilizohudhuria kongamano hilo lililofanyiaka katika
shule ya Msingi ya Kijitonyama Kisiwani
Shairi
mahususi likiimbwa na wanafunzi hao likiwa limebeba ujumbe wa kijana
jiepushe na matumizi ya Tumbaku na bidhaa zitokanazo na Tumbaku.
Mwanafunzi
wa darasa la tano, Tadei Ladislausi kutoka shule ya msingi Shekilango
(kulia)akisoma madhara yanayo wakumba watumiaji wa Tumbaku.
Wawili
kulia ni wanafunzi kutoka Chuo cha Afya Muhimbili, kushoto ni wanafunzi
wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani wakiwa wanasikiliza kwa makini
maada zilizo kuwa zikiendelea katika kongamano hilo.
Wanafunzi wakiuliza maswali kwa watoa mada inayo husiana na afya kwa kijana na kuepuka matumizi mabaya ya Tumbaku
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani, Bw. Charles Nombo akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali walioweza kuhudhuria katika kongamano hilo.
Mjumbe wa
Chama cha Afya ya Jamii Bi. Elizabeth Nchimbi akitoa nasaa kwa vijana
walioweza kuhudhuria na wale walioko nje wasiweze kutumia Tumbaku kwani
ni hatari kwa afya za binadamu
Waandhishi wa habari wakiwa kazini.
Afisa
Elimu kata ya Kijitonyama, Mwalimu Shangwe Temba akifunga kwa kutoa neno
kwa vijana kuacha kujiingiza katika makundi mbalimbali kwani ndio
yanayo pelekea vijana wengi kuhamasika na kuanza kutumia Tumbaku ambayo
huwaletea vijana wengi matatizo hususani kwa wanafunzi kuacha shule kwa
kuugua vifua vikuu na magonjwa mengine mengi
Picha ya umoja wa kikundi cha wanafunzi kinacho elimisha matumizi mabaya ya bidhaa zinazotokana na Tumbaku.
EmoticonEmoticon