Baadhi ya
Wanamichezo wa Polisi walioshiriki Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya
Polisi kusini mwa Afrika mwaka 2013 nchini Namibia wakiwa katika picha.
Timu za
Jeshi la Polisi Tanzania zitakazoshiriki michezo ya Umoja wa Wakuu wa
Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO), mwishoni mwa
mwezi julai nchini Swaziland zinaendelea kujifua vyema katika kambi yao
inayoendelea katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA).
Akizungumza
na blog hii Mkuu wa kitengo cha michezo cha Jeshi la Polisi, Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi SSP Jonas Mahanga alizitaja timu zilizopo kambini
kuwa ni pamoja na Timu ya Mpira wa miguu, pete, riadha na vishale ambapo
hivi sasa zinajifua kuhakikisha kuwa zinakuwa vizuri pindi michuano
hiyo itakapoanza kutimua vumbi.
Amesema
timu hizo zitaanza kucheza michezo ya kirafiki ili kujipima nguvu na
kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kuwa michezo ya mwaka huu itakuwa na
ushindani mkubwa kutokana na nchi zilizothibitisha kushiriki kujipanga
vizuri.
EmoticonEmoticon