Baadhi
ya wabunge wameitaka serikali kupambana na vyanzo vikubwa vya uhakika
vya kodi ikiwemo makampuni ya simu za mkononi badala ya kuongeza kodi
kwenye mafuta na kusababisha wananchi kuishi katika mazingira magumu.
Wakichangia mswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2015, baadhi ya wabunge wamehoji uwezo wa serikali wa kuyakabili makampuni makubwa ili yaweze kulipa kodi hususani katika mfumo wa soko huria ambapo baadhi ya makampni yamekuwa na mapato makubwa kuliko ya serikali.

Awali akiwasilisha maoni ya kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti,
Mheshimiwa Josephat Kandege amesema kutokana na kutokuwa na tafsiri
sahihi ya mafuta ghafi serikali imekuwa ikikosa mapato stahiki na
kuitaka kufanya uchunguzi, huku msemaji wa kambi ya upinzani Mhe.Joseph
Mbatia akiendelea kusisitiza kuwa kuongeza kodi katika mafuta
kutawaumiza wananchi.
Aidha akiwasilisha mswada wa sheria ya fedha hususani matumizi ya
sukari inayotumika viwandani, waziri wa fedha na uchumi Mhe Saada Mkuya
Salum amesema serikal imepunguza kodi hadi asilimia 25 kutoka asilimia
50 ya awali kwa waagizaji wa sukari ili kutoathiri mitaji ya
wafanyabiashara.
EmoticonEmoticon