Mkurugenzi
mtendaji wa wilaya ya Ikungi, Bwana Muhammad Nkya akiongea na wataalamu
waelekezi wa masuala ya mazingira na jinsia, kutoka kampuni ya CH2M
HILL ya Marekani Bi. Cinamon Vann na Bwana Piercarlo Smith (kushoto)
walipokuwa mkoani Singida kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa miradi ya
umeme inayotarajiwa kufadhiliwa na shirika la changamoto za millennia
(MCC), makubaliano ya ufadhili wa utekelezaji wa miradi hiyo kwa
Tanzania yanatarajiwa kufanyika mwezi Septemba 2015.
Mshauri
mwelekezi wa masuala ya jinsia ,kutoka kampuni ya CH2M HILL ya Marekani,
Bi. Cinamon Vann (wa pili kulia waliosimama), akiongea na wanawake wa
jamii ya kihadzabe na kimang'ati katika kijiji cha kipamba wilaya ya
Mkalama mkoani Singida walikokwenda kukusanya taarifa mbalimbali kwa
ajili ya upembuzi yakinifu wa miradi ya umeme inayotarajiwa kufadhiliwa
na Shirika la Changamoto za Millenia (MCC). Makubaliano ya ufadhili wa
utekelezaji wa miradi hiyo awamu ya pili kwa Tanzania yanatarajiwa
kufanyika mwezi Septemba 2015.
Mshauri
mwelekezi wa masuala ya jamii na mazingira ,kutoka kampuni ya CH2M HILL
ya Marekani, Bw. Piercarlo Smith (wa pili kushoto), akiongea na baadhi
ya wadau wa mazingira wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida
walikokwenda kukusanya taarifa mbalimbali kwa ajili ya upembuzi
yakinifu wa miradi ya umeme inayotarajiwa kufadhiliwa na Shirika la
Changamoto za Millenia (MCC). Makubaliano ya ufadhili wa utekelezaji wa
awamu ya pili wa miradi hiyo kwa Taanzania yanatarajiwa kufanyika mwezi
Septemba 2015
EmoticonEmoticon