Wakati
shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR likishindwa
kuwahamisha maelfu ya waomba hifadhi, hali ya usalama na hofu ya kutokea
kwa magonjwa ya mlipuko imewakumba waomba hifadhi kutoka Burundi ambao
wapo katika kijiji cha Kagunga wilayani Kigoma, baada ya idadi yao
kufikia zaidi ya elfu sitini huku kukiwa hakuna huduma za msingi katika
eneo hilo.
Wakizungumza
katika eneo hilo ambalo linakabiliwa na changamoto kadhaa zinazotishia
usalama kama kutokuwepo kwa maji safi na salama, huduma za afya, chakula
na mahema, wameomba kuhamishwa kutokana na hali mbaya iliyopo ambapo
kwa sasa hawana mahali pa kujificha mvua wala jua huku wakilazimika
kutumia maji ya ziwa Tanganyika kwa matumizi yote.
Huku
hali ikiwa mbaya katika kijiji hicho ambacho ndio kinapokea idadi kubwa
ya waomba hifadhi toka Burundi, ambao tangu April 26 mara tu baada ya
chama tawala nchini Burundi kumteua rais Pierre Nkurunziza kugombea tena
urais walianza kukimbia kutokana na hofu ya kutokea mapigano baada ya
kuwepo maandamano yanayoendelea katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura.
Shirika
la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR ambalo linatumia meli moja Mv
Liemba kuwahamishakatika kijiji hicho limeshidwa kutokanana idadi kubwa
ya waomba hifadhi wanaoingia kila siku katika kijiji hicho ambacho kipo
kandokando ya ziwa Tanganyika.
EmoticonEmoticon